Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 10:8 - Swahili Revised Union Version

8 Nao wakawasumbua na kuwaonea wana wa Israeli mwaka huo; waliwaonea wana wa Israeli wote waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani katika nchi ya Waamori, iliyoko huko Gileadi, muda wa miaka kumi na minane.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kwa miaka kumi na minane hao waliwatesa na kuwakandamiza Waisraeli walioishi huko Gileadi katika eneo la Waamori mashariki ya mto Yordani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kwa miaka kumi na minane hao waliwatesa na kuwakandamiza Waisraeli walioishi huko Gileadi katika eneo la Waamori mashariki ya mto Yordani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kwa miaka kumi na minane hao waliwatesa na kuwakandamiza Waisraeli walioishi huko Gileadi katika eneo la Waamori mashariki ya mto Yordani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 ambao waliowaonea na kuwatesa mwaka huo. Kwa miaka kumi na nane wakawatesa Waisraeli wote upande wa mashariki mwa Mto Yordani huko Gileadi, katika nchi ya Waamori.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 ambao waliwaonea na kuwatesa mwaka ule. Kwa miaka kumi na minane wakawatesa Waisraeli wote upande wa mashariki ya Mto Yordani katika Gileadi, nchi ya Waamori.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 10:8
7 Marejeleo ya Msalaba  

basi, uovu huu utakuwa kwenu kama mahali palipobomoka, kuanguka patokezapo katika ukuta mrefu, ambapo kuvunjika kwake huja ghafla kwa mara moja.


Na wana wa Makiri mwana wa Manase wakaenda Gileadi, na kuitwaa, na kuwapokonya Waamori waliokuwa humo.


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Yairi akafa, akazikwa huko Kamoni.


Hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, akawauza na kuwaua mikononi mwa Wafilisti, na mikononi mwa wana wa Amoni.


Wana wa Amoni nao wakavuka Yordani ili wapigane na Yuda, na kupigana na Benyamini, na nyumba ya Efraimu; basi hivyo Israeli walikuwa wanasumbuliwa sana.


Mkono wa Midiani ulikuwa na nguvu juu ya Israeli; tena kwa sababu ya Midiani wana wa Israeli walijifanyia hayo mashimo yaliyo milimani, na hayo mapango, na hizo ngome.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo