Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 16:7 - Swahili Revised Union Version

7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli, na haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Kisha, nikasikia sauti madhabahuni ikisema, “Naam, Bwana Mungu Mwenye Nguvu! Hukumu zako ni za kweli na haki!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Kisha, nikasikia sauti madhabahuni ikisema, “Naam, Bwana Mungu Mwenye Nguvu! Hukumu zako ni za kweli na haki!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Kisha, nikasikia sauti madhabahuni ikisema, “Naam, Bwana Mungu Mwenye Nguvu! Hukumu zako ni za kweli na haki!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nikasikia madhabahu ikiitikia, “Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni kweli na haki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nikasikia madhabahu ikiitikia, “Naam, bwana Mwenyezi Mungu, hukumu zako ni kweli na haki.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli, na haki.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 16:7
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha mmoja wa maserafi wale akaruka akanikaribia; naye alikuwa na kaa la moto mkononi mwake, ambalo alikuwa amelitwaa kwa makoleo toka juu ya madhabahu;


Naye akamwambia mtu yule aliyevaa bafta, akasema, Ingia kati ya magurudumu yazungukayo, yaani, chini ya kerubi, ukaijaze mikono yako yote miwili makaa ya moto, toka katikati ya makerubi, ukayamwage juu ya mji. Akaingia ndani mbele ya macho yangu.


Na kerubi yule akanyosha mkono wake toka katikati ya makerubi, kwa moto ule uliokuwa katikati ya makerubi, akatwaa baadhi ya moto ule, akautia katika mikono ya mtu yule aliyevaa bafta; naye akautwaa, akatoka.


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.


Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.


yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-kondoo.


Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana.


kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.


Na alipoufungua mhuri wa tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo