Obadia 1:21 - Swahili Revised Union Version21 Tena waokoaji watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya BWANA. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema21 Waokoaji watapanda juu ya mlima Siyoni ili kuutawala mlima Esau; naye Mwenyezi-Mungu atakuwa ndiye Mfalme.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND21 Waokoaji watapanda juu ya mlima Siyoni ili kuutawala mlima Esau; naye Mwenyezi-Mungu atakuwa ndiye Mfalme.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza21 Waokoaji watapanda juu ya mlima Siyoni ili kuutawala mlima Esau; naye Mwenyezi-Mungu atakuwa ndiye Mfalme.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu21 Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayuni kutawala milima ya Esau. Nao ufalme utakuwa wa Mwenyezi Mungu. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu21 Waokoaji watakwea juu ya Mlima Sayuni kutawala milima ya Esau. Nao ufalme utakuwa wa bwana. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI21 Tena waokoaji watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya BWANA. Tazama sura |
Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa joto; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa mamlaka ya kutoa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala kuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.