Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nehemia 12:1 - Swahili Revised Union Version

1 Basi, hawa ndio makuhani na Walawi waliopanda na Zerubabeli, mwana wa Shealueli, na Yoshua; Seraya, Yeremia, Ezra;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Ifuatayo ni orodha ya makuhani na Walawi waliorudi kutoka uhamishoni pamoja na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yeshua. Makuhani: Seraya, Yeremia, Ezra,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Ifuatayo ni orodha ya makuhani na Walawi waliorudi kutoka uhamishoni pamoja na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yeshua. Makuhani: Seraya, Yeremia, Ezra,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Ifuatayo ni orodha ya makuhani na Walawi waliorudi kutoka uhamishoni pamoja na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yeshua. Makuhani: Seraya, Yeremia, Ezra,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua: Seraya, Yeremia, Ezra,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hawa wafuatao walikuwa makuhani na Walawi ambao walirudi na Zerubabeli mwana wa Shealtieli pamoja na Yeshua: Seraya, Yeremia, Ezra,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Basi, hawa ndio makuhani na Walawi waliopanda na Zerubabeli, mwana wa Shealueli, na Yoshua; Seraya, Yeremia, Ezra;

Tazama sura Nakili




Nehemia 12:1
22 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtu wa Mungu.


Katika mwaka wa pili wa kufika kwao katika nyumba ya Mungu, huko Yerusalemu, mwezi wa pili, Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zao wengine, makuhani na Walawi, na watu wote, waliotoka katika uhamisho na kufika Yerusalemu, wakaanza; nao wakawaweka Walawi, hao wenye miaka ishirini na waliozidi, ili kuisimamia kazi ya nyumba ya BWANA.


wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa koo za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi tumemtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa.


Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.


Nao wakakwea baadhi ya wana wa Israeli, na wa makuhani, na wa Walawi, na waimbaji, na mabawabu, na Wanethini, ili kwenda Yerusalemu, katika mwaka wa saba wa mfalme Artashasta.


Na wa Walawi, wengine walikaa katika Yuda na wengine katika Benyamini.


Naye Yoshua akamzaa Yoyakimu, Yoyakimu akamzaa Eliashibu, Eliashibu akamzaa Yoyada,


Amaria, Maluki, Hatushi;


ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo idadi ya watu wa watu wa Israeli;


Katika mwaka wa pili wa utawala wa mfalme Dario, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la BWANA lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake nabii Hagai, kusema,


Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hao watu wote waliokuwa wamebaki, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA.


BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho za watu waliokuwa wamebaki; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao;


Sema sasa na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na hao watu waliokuwa wamebaki, ukisema,


naam, pokea fedha na dhahabu, ukatengeneze taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo