Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 2:11 - Swahili Revised Union Version

11 Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wanasimba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwanasimba, wala hapana aliyewatia hofu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Limekuwaje basi hilo pango la simba, hilo lililokuwa maficho ya wanasimba? Pamekuwaje hapo mahali pa simba, mahali pa wanasimba ambapo hakuna aliyeweza kuwashtua?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Liko wapi sasa pango la simba, ambapo waliwalisha watoto wao, ambapo simba dume na simba jike walienda, na wana simba pia, bila kuogopa chochote?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Liko wapi sasa pango la simba, mahali ambapo waliwalisha watoto wao, ambapo simba dume na simba jike walikwenda na ambapo wana simba walikwenda bila kuogopa chochote?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wanasimba pa wapi, mahali walipotembea simba dume na simba jike na mwanasimba, wala hapana aliyewatia hofu?

Tazama sura Nakili




Nahumu 2:11
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yuda ni mwanasimba, Kutoka katika mawindo, mwanangu, umepanda; Aliinama akajilaza kama simba, Na kama simba mke; ni nani atakayemwamsha?


Kwa sababu hiyo mikono yote italegea, na moyo wa kila mtu utayeyuka.


Maana BWANA aniambia hivi, Kama vile ilivyo simba angurumapo na mwanasimba juu ya mawindo yake, wachungaji wengi wakiitwa ili kumpiga, lakini hatiwi hofu na sauti zao, wala kufanya woga kwa sababu ya mshindo wao; ndivyo BWANA wa majeshi atakavyoshuka ili kufanya vita juu ya mlima Sayuni, na juu ya kilima chake.


Ngurumo yao itakuwa kama ya simba; Watanguruma kama wanasimba; Naam, watanguruma na kukamata mateka, Na kuyachukua na kwenda zao salama, Wala hakuna mtu atakayeokoa.


Wanasimba wamenguruma juu yake, wametoa sana sauti zao; Nao wameifanya nchi yake kuwa ukiwa; miji yake imeteketea, haina watu.


Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa; ameanza kushika njia, ametoka katika mahali pake; ili aifanye nchi yako kuwa ukiwa, miji yako ifanywe maganjo, asibaki mwenyeji ndani yake.


Israeli ni kondoo aliyetawanywa; simba wamemfukuzia mbali; kwanza mfalme wa Ashuru amemla, na mwisho Nebukadneza huyu, mfalme wa Babeli, amemvunja mifupa yake.


Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?


Mwanadamu, mfanyie Farao, mfalme wa Misri, maombolezo, umwambie, Ulifananishwa na mwanasimba wa mataifa; lakini umekuwa kama joka katika bahari; nawe watoka kwa nguvu pamoja na mito yako, na kuyachafua maji kwa miguu yako, na kuitia uchafu mito yao.


Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu.


Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.


Simba alirarua vipande vipande chakula cha kuwatosha watoto wake, aliwakamatia majike wake mawindo, aliyajaza mapango yake mateka, na makao yake aliyajaza nyama iliyoraruliwa.


Ole wake mji wa damu! Umejaa mambo ya uongo na unyang'anyi; mateka hayaondoki.


Wakuu wake walio ndani yake ni simba wangurumao; mahakimu wake ni mbwamwitu wa jioni; wasiobakiza kitu chochote mpaka asubuhi.


Tazama, watu hawa wanaondoka kama simba jike, Na kama simba anajiinua nafsi yake, Hatalala hadi atakapokula mawindo, Na kunywa damu yao waliouawa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo