Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 50:13 - Swahili Revised Union Version

13 kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, na wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Wakamchukua hadi nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Ibrahimu alilinunua kutoka kwa Efroni Mhiti pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Ibrahimu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, na wakamzika katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, alilonunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 50:13
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na lile shamba, na pango lililomo, iliyakinishwa kuwa mali yake Abrahamu na wazawa wa Hethi, kuwa mahali pa kuzikia.


ili kwamba anipe pango la Makpela, iliyo katika mpaka wa shamba lake, na anipe kwa kima kilicho kamili, katikati yenu, iwe milki yangu ya kuzikia.


Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.


Isaka na Ishmaeli wanawe wakamzika katika pango ya Makpela, katika shamba la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, lielekealo Mamre.


Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Abrahamu na Isaka.


Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.


Mimi nitashuka pamoja nawe mpaka Misri; nami nitakupandisha tena bila shaka; na Yusufu ataweka mkono wake juu ya macho yako.


Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema.


Wanawe wakamfanyia kama alivyowaagiza;


Yusufu akarudi Misri, yeye na ndugu zake, na wote waliokwenda pamoja naye kumzika baba yake, baada ya kumzika baba yake.


Manase akalala na babaze, akazikwa katika bustani ya nyumba yake mwenyewe, yaani, bustani ya Uza. Na Amoni mwanawe akatawala mahali pake.


wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Abrahamu alilinunua kwa kima fulani cha fedha kutoka kwa wana wa Hamori, huko Shekemu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo