Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 45:16 - Swahili Revised Union Version

16 Habari ikasikika nyumbani mwa Farao kusema, Ndugu zake Yusufu wamekuja. Ikawa vema machoni pa Farao, na machoni pa watumishi wake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Habari hizo zilipofika ikulu ya mfalme, kwamba ndugu za Yosefu wamekuja, zikamfurahisha sana Farao na watumishi wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Habari hizo zilipofika ikulu ya mfalme, kwamba ndugu za Yosefu wamekuja, zikamfurahisha sana Farao na watumishi wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Habari hizo zilipofika ikulu ya mfalme, kwamba ndugu za Yosefu wamekuja, zikamfurahisha sana Farao na watumishi wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Habari zilipofika kwenye jumba la Farao kwamba ndugu zake Yusufu wamefika, Farao na maafisa wake wote wakafurahi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Habari zilipofika kwenye jumba la Farao kwamba ndugu zake Yusufu wamefika, Farao na maafisa wake wote wakafurahi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Habari ikasikika nyumbani mwa Farao kusema, Ndugu zake Yusufu wamekuja. Ikawa vema machoni pa Farao, na machoni pa watumishi wake.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 45:16
15 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mikononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.

Abimeleki akasema, Nchi yangu iko mbele yako, ishi upendapo.

Maneno yao yakawa mema machoni pa Hamori, na machoni pa Shekemu, mwana wa Hamori.

Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.

Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumishi wake wote.

Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye.

Farao akamwambia Yusufu, Uwaambie ndugu zako, Fanyeni hivi; wabebesheni mizigo wanyama wenu, mwondoke mwende nchi ya Kanaani;

Wakaangalia watu wote, yakawa mema machoni pao; kama yalivyokuwa mema machoni pao yote aliyoyatenda mfalme.

Likawa neno jema machoni pa mfalme, na kusanyiko lote.

Basi neno hili likawapendeza mfalme na wakuu wake; naye mfalme akafanya kama alivyopendekeza Memukani.

Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti. Neno hilo likampendeza mfalme, naye akafanya hivyo.

Basi Zereshi mkewe na marafiki wote wa Hamani wakamwambia, Na kitengenezwe kiunzi cha mti wa kunyongea wa urefu wa mikono hamsini, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa furaha pamoja na mfalme karamuni. Basi ushauri huu ukamridhisha Hamani, akautengeneza mti wa kunyongea.

Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;

Hata safari ya pili Yusufu akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusufu ikawa dhahiri kwa Farao.

aliyewatangulia njiani, usiku kwa moto, kuwaonesha njia mtakayoiendea, na mchana kwa hilo wingu, ili apate kuwatafutia mahali pa kusimamisha hema zenu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo