Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 45:15 - Swahili Revised Union Version

15 Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Akiwa bado analia, Yosefu akawakumbatia ndugu zake na kuwabusu. Hapo ndipo ndugu zake walipoweza kuzungumza naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Akiwa bado analia, Yosefu akawakumbatia ndugu zake na kuwabusu. Hapo ndipo ndugu zake walipoweza kuzungumza naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Akiwa bado analia, Yosefu akawakumbatia ndugu zake na kuwabusu. Hapo ndipo ndugu zake walipoweza kuzungumza naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Pia akawabusu ndugu zake wote, huku akilia. Baada ya hayo, ndugu zake wakazungumza naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Pia akawabusu ndugu zake wote, huku akilia. Baada ya hayo ndugu zake wakazungumza naye.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Akawabusu ndugu zake wote, akalia nao, baada ya hayo, nduguze wakazungumza naye.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 45:15
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akambusu Raheli, akalia kwa sauti.


Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.


Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia.


Akaenda kando, akalia. Kisha akawarudia, na kusema nao, akamtwaa Simeoni miongoni mwao, akamfunga mbele ya macho yao.


Akaanguka shingoni mwa ndugu yake Benyamini, akalia; Benyamini naye akalia shingoni mwake.


Habari ikasikika nyumbani mwa Farao kusema, Ndugu zake Yusufu wamekuja. Ikawa vema machoni pa Farao, na machoni pa watumishi wake.


Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia.


Yusufu akatandika gari lake, akapanda kwenda kumlaki Israeli, babaye, huko Gosheni; akajionesha kwake, akamwangukia shingoni, akalia shingoni mwake kitambo kirefu.


Basi Yoabu akamwendea mfalme, akamwambia hayo, naye alipomwita Absalomu, yeye akaja kwa mfalme, akainama kifudifudi hadi chini mbele ya mfalme; naye mfalme akambusu Absalomu.


Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena.


BWANA akamwambia Haruni, Nenda jangwani uonane na Musa. Naye akaenda, akamkuta katika mlima wa Mungu, akambusu.


Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa bado mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu.


Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusubusu,


Nao wakapaza sauti zao, wakalia tena, na Orpa akambusu mkwewe, lakini Ruthu akaambatana naye.


BWANA na awajalie kuona raha kila mmoja nyumbani kwa mumewe. Kisha akawabusu; nao wakapaza sauti zao wakalia.


Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.


Basi mara alipokuwa amekwisha ondoka yule mtoto, mara Daudi akatoka mahali pale karibu na kile kichuguu, akaanguka kifudifudi, akajiinama mara tatu; nao wakabusiana, wakaliliana, hata Daudi akazidi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo