Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 39:5 - Swahili Revised Union Version

5 Ikawa tokea wakati alipomweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Baraka za BWANA zikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Tokea wakati Potifa alipomfanya Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba yake na mwangalizi wa mali yake, Mwenyezi-Mungu akaibariki nyumba ya huyo Mmisri kwa ajili ya Yosefu. Baraka za Mwenyezi-Mungu zikawa juu ya kila alichokuwa nacho, nyumbani na shambani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Tokea wakati Potifa alipomfanya Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba yake na mwangalizi wa mali yake, Mwenyezi-Mungu akaibariki nyumba ya huyo Mmisri kwa ajili ya Yosefu. Baraka za Mwenyezi-Mungu zikawa juu ya kila alichokuwa nacho, nyumbani na shambani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yusufu kuwa msimamizi wa nyumba na mali yake yote aliyokuwa nayo, Mwenyezi Mungu aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yusufu. Baraka ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yusufu kuwa msimamizi wa nyumba na mali zake zote alizokuwa nazo, bwana aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yusufu. Baraka ya bwana ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Ikawa tokea wakati alipomweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, na vyote vilivyomo, BWANA akabariki nyumba ya yule Mmisri kwa ajili ya Yusufu. Baraka za BWANA zikawa juu ya vyote alivyokuwa navyo katika nyumba, na katika shamba.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 39:5
9 Marejeleo ya Msalaba  

nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.

Labani akamwambia, Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba BWANA amenibariki kwa ajili yako.

Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.

Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.

akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.

Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo