Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 3:8 - Swahili Revised Union Version

8 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Jioni, wakati wa kupunga upepo, huyo mwanamume na mkewe wakasikia hatua za Mwenyezi-Mungu akitembea bustanini, nao wakajificha kati ya miti ya bustani, Mwenyezi-Mungu asipate kuwaona.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Yule mwanaume na mkewe waliposikia sauti ya Bwana Mwenyezi Mungu akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka kwa Bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya bwana Mwenyezi Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za bwana Mwenyezi Mungu katikati ya miti ya bustani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 3:8
20 Marejeleo ya Msalaba  

Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.


Akasema, Nilisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.


Mawingu mazito ni kifuniko chake, hata asione; Naye yuatembea juu ya kuba ya mbingu.


Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;


Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,


Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.


Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.


Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.


Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.


Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa BWANA; akateremka hadi Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akalipa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa BWANA.


Hao waionesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;


kwa kuwa BWANA. Mungu wako, yuatembea katika kituo akuokoe, na kukutolea adui zako mbele yako; kwa hiyo na kiwe kitakatifu kituo chako; asije akaona kitu kwako kisichokuwa safi, akageuka na kukuacha.


Je! Kuna wakati wowote watu wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, na wakaendelea kuishi?


Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa.


Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.


Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na muungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo