Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 24:44 - Swahili Revised Union Version

44 naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia wako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke BWANA aliyemwekea mwana wa bwana wangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

44 naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

44 naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

44 naye akanipa na kuwatekea maji ngamia wangu, basi huyo na awe ndiye uliyemchagua kuwa mke wa mwana wa bwana wangu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

44 Naye akiniambia, “Kunywa, nami nitawatekea ngamia wako maji pia,” basi huyo awe ndiye mke Mwenyezi Mungu amemchagulia mwana wa bwana wangu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

44 naye kama akiniambia, “Kunywa, nami nitateka maji kwa ajili ya ngamia wako pia,” basi huyo awe ndiye mke ambaye bwana amemchagulia mwana wa bwana wangu.’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

44 naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia wako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke BWANA aliyemwekea mwana wa bwana wangu.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 24:44
11 Marejeleo ya Msalaba  

na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.


basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu.


tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji; basi na iwe hivi, msichana ajaye kuteka maji, nikamwambia, Nipe, nakuomba, maji kidogo katika mtungi wako ninywe,


Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama! Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe.


Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.


Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA.


Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.


Bali muungwana huwaza mambo ya kiungwana, naye hushika sana mambo ya kiungwana.


bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.


Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.


Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo