Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 19:5 - Swahili Revised Union Version

5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wako wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwalete kwetu, ili tuweze kuwajua kimwili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Wakamwita Loti na kumwuliza, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako? Watoe nje. Tunataka kulala nao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Wakamwita Lutu wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuwalawiti.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Wakamwita Lutu wakisema, “Wako wapi wale watu ambao walikuja kwako jioni hii? Watoe nje kwetu ili tuweze kuwalawiti.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wako wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwalete kwetu, ili tuweze kuwajua kimwili.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 19:5
23 Marejeleo ya Msalaba  

Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake.


Na mahanithi walikuwako katika nchi, wakafanya sawasawa na machukizo yote ya mataifa BWANA aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.


Tena mahanithi waliosalia, hao waliosalia siku za Asa baba yake, akawaondoa katika nchi.


Kama BWANA wa majeshi asingalituachia mabaki machache sana, tungalikuwa kama Sodoma, tungalifanana na Gomora.


Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu yao, wafunua dhambi yao kama Sodoma, hawaifichi. Ole wa nafsi zao, kwa maana wamejilipa nafsi zao uovu.


Kwa sababu hiyo manyunyu yamezuiliwa, wala hapakuwa na mvua ya vuli; hata hivyo ulikuwa na kipaji cha uso cha kahaba, ulikataa kutahayarika.


Je! Walitahayarika, walipokuwa wameunda machukizo? La, hawakutahayarika hata kidogo, wala hawakuweza kuona haya usoni; basi, wataanguka miongoni mwa hao waangukao; wakati nitakapowajia wataangushwa chini, asema BWANA.


Tazama, uovu wa dada yako, Sodoma, ulikuwa huu; kiburi, na kushiba chakula, na kufanikiwa, hayo yalikuwa ndani yake na binti zake; lakini hukuwasaidia maskini na wahitaji.


Nao walijivuna, wakafanya machukizo mbele zangu; kwa sababu hiyo niliwaondoa hapo nilipoyaona.


Samaria naye hakutenda nusu ya dhambi zako; bali wewe umeyaongeza machukizo yako zaidi ya hao, nawe umewapa haki dada zako kwa machukizo yako yote uliyoyatenda.


Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.


Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,


Pasiwe na kahaba katika binti za Israeli, wala pasiwe na hanithi katika wana wa Israeli wanaume.


na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;


Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.


Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa.


akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu;


Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kandokando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.


Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo