Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 16:2 - Swahili Revised Union Version

2 Sarai akamwambia Abramu, kwa kuwa BWANA amenifunga tumbo nisizae, sasa mwingilie mjakazi wangu, labda nitapata uzao kutoka kwake. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, Sarai akamwambia Abramu, “Unajua kuwa Mwenyezi-Mungu hajanijalia kupata watoto. Mchukue Hagari mjakazi wangu; huenda nikapata watoto kwake.” Abramu akakubali shauri la Sarai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Mwenyezi Mungu amenizuilia kupata watoto. Basi nenda ukutane kimwili na mjakazi wangu; huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 hivyo Sarai akamwambia Abramu, “bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.” Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Sarai akamwambia Abramu, kwa kuwa BWANA amenifunga tumbo nisizae, sasa mwingilie mjakazi wangu, labda nitapata uzao kutoka kwake. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 16:2
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.

Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa makabila ya watu watatoka kwake.

Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mwanamume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.

Maana BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Abrahamu.

Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.

Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;

Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.

Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.

Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.

Ikiwa ni bwana wake aliyemwoza huyo mke, naye amemzalia wana, wa kiume au wa kike; yule mke na wanawe watakuwa ni mali ya bwana wake, naye mume atatoka peke yake.

Na watu wote waliokuwapo langoni, na wale wazee, wakasema, Naam, sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wawili walioijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrata, na kuwa mashuhuri katika Bethlehemu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo