Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 13:5 - Swahili Revised Union Version

5 Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kadhalika, Loti, ambaye alifuatana na Abramu, alikuwa na kondoo, mifugo na hema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kadhalika, Loti, ambaye alifuatana na Abramu, alikuwa na kondoo, mifugo na hema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kadhalika, Loti, ambaye alifuatana na Abramu, alikuwa na kondoo, mifugo na hema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Basi Lutu, aliyekuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na mifugo na mahema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Basi Lutu, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ng’ombe na mahema.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Na Lutu aliyesafiri pamoja na Abramu, yeye naye alikuwa na makundi ya ng'ombe na kondoo, na hema.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 13:5
6 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Abramu akaenda, kama BWANA alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.


Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.


Na ile nchi haikuwatosha, ili wakae pamoja; maana mali zao zilikuwa nyingi, hata wasiweze kukaa pamoja.


Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa hemani.


Ada akamzaa Yabali; huyo ndiye baba yao wakaao katika hema na kufuga wanyama.


Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia wao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo