Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mika 4:13 - Swahili Revised Union Version

13 Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mwenyezi-Mungu asema, “Enyi watu wa Siyoni, inukeni mkawaadhibu adui zenu! Nitawapeni nguvu kama fahali mwenye pembe za chuma na kwato za shaba. Mtawasaga watu wa mataifa mengi; mapato yao mtaniwekea wakfu mimi, mali zao mtanitolea mimi Bwana wa dunia yote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Inuka upure, ee Binti Sayuni, kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; nitakupa kwato za shaba na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa Mwenyezi Mungu, utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Inuka upure, ee Binti Sayuni, kwa kuwa nitakupa pembe za chuma; nitakupa kwato za shaba na utavunja vipande vipande mataifa mengi.” Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwa bwana, utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.

Tazama sura Nakili




Mika 4:13
28 Marejeleo ya Msalaba  

Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake.


Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu Wafalme watakuletea hedaya.


Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.


Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hidaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inagawanya nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.


Ewe wangu niliyekufikicha na kukupura; Hayo niliyoyasikia kwa BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, nayatangaza kwenu.


Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.


Mishale yao ni mikali, na pinde zao zote zimepindika; Kwato za farasi wao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;


Wewe ni rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;


Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake.


Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.


Naye Efraimu ni ndama aliyefundishwa, apendaye kupura; lakini nimepitisha kongwa juu ya shingo yake nzuri; nitampandisha mwenye kupanda juu ya Efraimu; Yuda atalima, na Yakobo atapiga haro yeye mwenyewe.


Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika nyasi; yasiyowategemea watu, wala kuwangojea wanadamu.


Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira.


Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata majeraha mengi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.


Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kulia na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.


Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili watiwa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.


Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote.


Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;


Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.


Lakini fedha yote, na dhahabu, na vyombo vya shaba, na chuma, ni vitakatifu kwa BWANA; vitaletwa katika hazina ya BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo