Basi hayo yote yalipokwisha, Israeli wote waliokuwako wakatoka waende miji ya Yuda, wakazivunjavunja nguzo, wakayakatakata Maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hadi walipoviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao.