Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mhubiri 1:14 - Swahili Revised Union Version

14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Nimeyaona yote yanayofanywa duniani; yote ni bure: Ni sawa na kufukuza upepo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Nimeyaona yote yanayofanywa duniani; yote ni bure: Ni sawa na kufukuza upepo!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Nimeyaona yote yanayofanywa duniani; yote ni bure: ni sawa na kufukuza upepo!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Nimeshaona mambo yote yanayotendeka chini ya jua, hayo yote ni ubatili, hii ni kukimbiza upepo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Nimeshaona mambo yote yanayotendeka chini ya jua, hayo yote ni ubatili, hii ni kukimbiza upepo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.

Tazama sura Nakili




Mhubiri 1:14
13 Marejeleo ya Msalaba  

Mhubiri asema, Ubatili mtupu; mambo yote ni ubatili!


Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kufukuza upepo, wala faida hakuna chini ya jua.


Basi, nikauchukia uhai; kwa sababu kazi inayotendeka chini ya jua ilikuwa mbaya kwangu; yaani, mambo yote ni ubatili na kufukuza upepo.


Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.


Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kufukuza upepo.


Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.


Heri kuona kwa macho, Kuliko kutangatanga kwa tamaa. Hayo nayo ni ubatili, na kufukuza upepo.


Mimi nilipotia moyo wangu katika kuijua hekima, na kuuona utumishi uliofanyika juu ya nchi, (maana kuna asiyepata usingizi kwa macho yake mchana wala usiku);


Tufuate:

Matangazo


Matangazo