Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:9 - Swahili Revised Union Version

9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Heri walio wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:9
31 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Daudi akatoka ili kuwalaki, akajibu, akawaambia, Kama mmenijia kwa amani ili kunisaidia, basi nitawapokea kwa moyo wote; lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu, ingawa hamna udhalimu mikononi mwangu, Mungu wa baba zetu na alitazame neno hili, na kulikemea.


Kwa muda mrefu nimeishi, Pamoja na watu wanaoichukia amani.


Ni nani atamaniye uzima na atakaye kuishi, Siku nyingi afurahie mema?


ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.


Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.


Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.


Kesho yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana?


Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.


Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.


Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;


Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.


Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini.


Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.


Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu.


Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;


Namsihi Euodia, namsihi na Sintike, wawe na nia moja katika Bwana.


mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.


Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo