Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 2:15 - Swahili Revised Union Version

15 akakaa huko hadi Herode alipokufa; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nilimwita mwanangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 ambako walikaa hadi Herode alipofariki. Hili lilifanyika ili litimie lile neno Mwenyezi Mungu alilosema kupitia kwa nabii: “Nilimwita mwanangu kutoka Misri.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 ambako walikaa mpaka Herode alipofariki. Hili lilifanyika ili litimie lile lililonenwa na Mwenyezi Mungu kwa kinywa cha nabii, kusema: “Nilimwita mwanangu kutoka Misri.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 akakaa huko hadi Herode alipokufa; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nilimwita mwanangu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 2:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;


Israeli alipokuwa mtoto, nilikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri.


Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake.


Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,


Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri;


Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,


Herode alipofariki, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri,


akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazareti.


Haya yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema,


Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?


Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.


Walipokwisha kumsulubisha, waligawana mavazi yake, kwa kupiga kura; [ili litimie neno lililonenwa na nabii, Waligawa nguo zangu kati yao, na juu ya vazi langu walipiga kura.]


ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.


Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa ningali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika vitabu vya Manabii na Zaburi.


Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.


Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa.


Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo