Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 10:14 - Swahili Revised Union Version

14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakunguteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Kama mtu yeyote atakataa kuwakaribisheni au kuwasikilizeni, basi mtokapo katika nyumba hiyo au mji huo, yakung'uteni mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Na mtu asipowakaribisha wala kuyasikiliza maneno yenu, mtokapo katika nyumba ile, au mji ule, kung'uteni mavumbi ya miguuni mwenu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:14
14 Marejeleo ya Msalaba  

Tena nikakung'uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung'ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung'utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.


Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.


Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;


Na mahali popote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao.


Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.


akawaambia, Yeyote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na yeyote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.


Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung'uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimtumaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenituma.


Nao wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.


Walipopingana naye na kumtukana Mungu, akakung'uta mavazi yake, akawaambia, Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu; mimi ni safi; tangu sasa nitakwenda kwa watu wa Mataifa.


Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo