Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Maombolezo 3:56 - Swahili Revised Union Version

56 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

56 Wewe umenisikia nikikulilia: ‘Usiache kusikia kilio changu cha msaada bali unipatie nafuu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

56 Wewe umenisikia nikikulilia: ‘Usiache kusikia kilio changu cha msaada bali unipatie nafuu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

56 Wewe umenisikia nikikulilia: ‘Usiache kusikia kilio changu cha msaada bali unipatie nafuu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

56 Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

56 Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

56 Ukaisikia sauti yangu; usifiche sikio lako Ili usisikie pumzi yangu, kwa kilio changu.

Tazama sura Nakili




Maombolezo 3:56
17 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu.


Sala yake pia, na jinsi Mungu alivyomtakabali, na dhambi yake yote, na kosa lake, na mahali alipopajenga mahali pa juu, na kupasimamishia Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeza; tazama, hayo yameandikwa katika Kumbukumbu ya Hozai.


Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.


Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.


Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.


Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.


BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.


Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche nikuombapo rehema.


Ameiokoa nafsi yangu iwe salama, asinikaribie mtu, Maana walioshindana nami walikuwa wengi.


Unisikilize na kunijibu, Nimetangatanga nikilalama na kuugua.


Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.


Nenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.


Basi sasa, Ee Mungu wetu, yasikilize maombi ya mtumishi wako, na dua zake, ukaangazishe uso wako juu ya patakatifu pako palipo ukiwa, kwa ajili ya Bwana.


Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo