Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Luka 5:34 - Swahili Revised Union Version

34 Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa arusini, akiwapo bwana arusi pamoja nao?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Yesu akawajibu, “Je, wale walioalikwa harusini hutakiwa wafunge hali bwana arusi yuko pamoja nao? La!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Yesu akawajibu, “Je, wale walioalikwa harusini hutakiwa wafunge hali bwana arusi yuko pamoja nao? La!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Yesu akawajibu, “Je, wale walioalikwa harusini hutakiwa wafunge hali bwana arusi yuko pamoja nao? La!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Isa akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Isa akawajibu, “Je, mnaweza kuwafanya wageni wa bwana arusi kufunga wakati yuko pamoja nao?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

34 Lakini Yesu akawaambia, Je! Mwaweza kuwafanya wafunge walioalikwa harusini, akiwapo bwana harusi pamoja nao?

Tazama sura Nakili




Luka 5:34
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi.


Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe?


Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.


Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.


BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa; Atakushangilia kwa furaha kuu, Atakutuliza katika upendo wake, Atakufurahia kwa kuimba.


Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.


Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga.


Nao wakamwambia, Wanafunzi wa Yohana hufunga mara nyingi, na kuomba dua; na kadhalika wanafunzi wa Mafarisayo; lakini wanafunzi wako hula na kunywa!


Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi, ndipo watakapofunga siku zile.


Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.


Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa niliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo