Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 13:5 - Swahili Revised Union Version

5 Itakuwa hapo BWANA atakapowaleta mpaka nchi ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Wahivi, na Wayebusi, nchi hiyo aliyowaapia baba zako kwamba atakupa wewe, ni nchi imiminikayo maziwa na asali, ndipo mtakapoushika utumishi huu katika mwezi huu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Na wakati Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa nyinyi, nchi inayotiririka maziwa na asali, ni lazima muiadhimishe sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Na wakati Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa nyinyi, nchi inayotiririka maziwa na asali, ni lazima muiadhimishe sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Na wakati Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi ambayo aliwaapia babu zenu kwamba atawapa nyinyi, nchi inayotiririka maziwa na asali, ni lazima muiadhimishe sikukuu hii kila mwaka katika mwezi huu wa kwanza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mwenyezi Mungu atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi inayotiririka maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 bwana atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Wahivi na Wayebusi, nchi aliyowaapia baba zako kukupa, nchi itiririkayo maziwa na asali, utaiadhimisha sikukuu hii katika mwezi huu:

Tazama sura Nakili




Kutoka 13:5
31 Marejeleo ya Msalaba  

Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.


Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.


na Mhivi, na Mwarki, na Msini;


Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele.


Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.


Itakuwa hapo BWANA atakapokuleta katika nchi ya Wakanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, na kukupa,


Nami nimesema, Nitawapandisha kutoka katika mateso ya Misri na kuwaingiza katika nchi ya Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, nchi ijaayo maziwa na asali.


nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.


Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.


BWANA akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii;


Liangalie neno hili ninalokuamuru leo; tazama, mbele yako namtoa Mwamori, na Mkanaani, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.


Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya waliyokaa kama wageni.


Nami nitawaleta hata nchi ile ambayo niliinua mkono wangu, niwape Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; nitawapa iwe urithi wenu; Mimi ni YEHOVA.


ili nipate kukitimiza kiapo nilichowaapia baba zenu, kuwapa nchi itiririkayo maziwa na asali, kama ilivyo hivi leo. Ndipo nikajibu, nikasema, Amina, Ee BWANA.


ukawapa nchi hii, uliyowaapia baba zao kwamba utawapa, nchi itiririkayo maziwa na asali;


katika siku ile niliwainulia mkono wangu, kuwatoa katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyowapelelezea, itiririkayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote;


Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni BWANA, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.


Je! Ni mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote je! Ni mimi niliyewazaa, hata ikawa wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea achukuavyo mtoto anyonyaye, uende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao?


Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile uliyotutuma, kwa hakika, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, uthibitisho, haya ndiyo matunda yake.


Ni kwa sababu yeye BWANA hakuweza kuwaleta watu hao kuwatia katika nchi aliyowaapia, kwa ajili ya hayo amewaua nyikani.


hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliapa kwa kuinua mkono wangu, kwamba nitawafanyia makao humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.


Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote;


BWANA, Mungu wako, atakapoyaondolea mbali hayo mataifa mbele yako, huko uingiako kuyamiliki, nawe ukawatwaa, na kuishi katika nchi yao;


BWANA, Mungu wako, atakapoyakatilia mbali hayo mataifa yenye nchi akupayo BWANA, Mungu wako, nawe ukawafuata, na kukaa katika miji yao, na katika nyumba zao;


Na itakuwa, ukiisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako, iwe urithi, na kuimiliki, na kukaa ndani yake;


BWANA, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe;


Nanyi mliuvuka Yordani, mkafika Yeriko; nao watu wa Yeriko wakapigana nanyi, Mwamori, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhiti, na Mgirgashi, na Mhivi, na Myebusi; nami nikawatia mikononi mwenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo