Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 60:9 - Swahili Revised Union Version

9 Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Hakika visiwa vinanitazama; merikebu za Tarshishi ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Hakika visiwa vinanitazama, merikebu za Tarshishi ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya bwana, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.

Tazama sura Nakili




Isaya 60:9
46 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu amwongezee Yafethi. Na akae katika hema za Shemu; Na Kanaani awe mtumwa wake.


Na malkia wa Sheba aliposikia habari za Sulemani juu ya jina la BWANA, alikuja ili amjaribu kwa maswali ya fumbo.


Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.


Yehoshafati akafanya merikebu za Tarshishi ziende Ofiri kuchukua dhahabu; lakini hazikuenda; kwa maana merikebu zilivunjika huko Esion-geberi.


Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako;


Kama upepo wa mashariki Unapovunja jahazi za Tarshishi.


Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.


BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.


Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.


Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.


Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.


na juu ya merikebu zote za Tarshishi, na juu ya kila taswira ipendezayo.


Basi, mtukuzeni BWANA katika mashariki, litukuzeni jina la BWANA, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.


Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Na sifa zake tokea mwisho wa dunia; Ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, Na visiwa, nao wakaao humo.


Hatazimia, wala hatakata tamaa, hata atakapoweka hukumu duniani; na visiwa vitaingojea sheria yake.


Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na makabila ya watu kwa ajili ya maisha yako.


nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.


Mimi ninaleta karibu haki yangu, haitakuwa mbali, na wokovu wangu hautakawia; nami nitaweka wokovu katika Sayuni kwa ajili ya Israeli, utukufu wangu.


Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.


Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwainulia makabila ya watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.


Haki yangu i karibu, wokovu wangu umekuwa wazi, na mikono yangu itawahukumu makabila ya watu; visiwa vitaningoja, navyo vitautumainia mkono wangu.


Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.


Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake niliona hasira, nikampiga; nilificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.


Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani.


Wingi wa ngamia utakufunika, Ngamia vijana wa Midiani na Efa; Wote watakuja kutoka Sheba; Wataleta dhahabu na uvumba; Na kuzitangaza sifa za BWANA.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha BWANA; na mataifa yote yatakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la BWANA; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya.


Tena kwao itasikiwa shukrani, na sauti yao wachangamkao; nami nitawazidisha, wala hawatakuwa wachache; tena nitawatukuza, wala hawatakuwa wanyonge.


Na jina langu takatifu nitalifanya kuwa limejulikana kati ya watu wangu Israeli; wala sitaliacha jina langu takatifu kutiwa unajisi tena; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, na Aliye Mtakatifu katika Israeli.


Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.


Siku hiyo watakujia kutoka Ashuru na miji ya Misri, na kutoka Misri mpaka huo Mto, na kutoka bahari hii mpaka bahari hii, na kutoka mlima huu mpaka mlima huu.


BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.


Yuda naye atafanya vita juu ya Yerusalemu; na huo utajiri wa mataifa wa pande zote utakusanywa, dhahabu, na fedha, na mavazi; vitu vingi sana.


Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Nami niliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.


Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.


Bali Yerusalemu wa juu ni muungwana, naye ndiye mama yetu sisi.


Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako tunatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la BWANA, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo