Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 47:14 - Swahili Revised Union Version

14 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa kutoka kwa nguvu za muali wa moto; hili halitakuwa kaa la kujipasha moto, wala moto wa kuota.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 “Kumbuka, wao ni kama mabua makavu: Moto utayateketezea mbali! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 “Kumbuka, wao ni kama mabua makavu: Moto utayateketezea mbali! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 “Kumbuka, wao ni kama mabua makavu: moto utayateketezea mbali! Hawawezi hata kujiokoa wenyewe mbali na ukali wa moto huo. Moto huo si wa kujipatia joto, huo si moto wa kuota!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Hakika wako kama mabua makavu; moto utawateketeza. Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe kutokana na nguvu za mwali wa moto. Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto; hapa hakuna moto wa kuota.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Hakika wako kama mabua makavu; moto utawateketeza. Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe kutokana na nguvu za mwali wa moto. Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto; hapa hakuna moto wa kuota.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa kutoka kwa nguvu za muali wa moto; hili halitakuwa kaa la kujipasha moto, wala moto wa kuota.

Tazama sura Nakili




Isaya 47:14
21 Marejeleo ya Msalaba  

Basi hao watu wakatawanyika katika nchi yote ya Misri ili wapate kukusanya takataka ya mashamba badala ya majani.


Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa muali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake kwa siku moja.


Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.


Wenye dhambi walio katika Sayuni wanaogopa; tetemeko limewashika wasiomcha Mungu; Ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uangamizao; ni nani kwetu sisi awezaye kukaa na moto uteketezao milele?


Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.


Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? Ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake.


Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto;


Kwa hiyo kama vile muali wa moto uteketezavyo mabua makavu, na kama manyasi makavu yaangukavyo katika muali wa moto; kadhalika shina lao litakuwa kama ubovu, na ua lao litapeperushwa juu kama mavumbi; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA wa majeshi, na kulidharau neno lake aliye Mtakatifu wa Israeli.


Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana; Wanakaa katika ngome zao; Ushujaa wao umewapungukia; Wamekuwa kama wanawake; Makao yake yameteketea; Makomeo yake yamevunjika.


Navyo vivuko vimeshambuliwa, Nayo makangaga wameyatia moto, Nao watu wa vita wameingiwa na hofu.


BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.


Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.


Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto iunguzapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita.


Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa muali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa BWANA amesema hayo.


Kwa maana kama miiba wametatana, kama walevi wamelewa, watateketezwa kama mabua makavu.


Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.


Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.


Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?


Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo