Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 38:20 - Swahili Revised Union Version

20 BWANA yu tayari kunipa wokovu. Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu, Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 “Mwenyezi-Mungu ataniokoa. Nasi tutamsifu kwa nyimbo za vinubi siku zote za maisha yetu, nyumbani kwake Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 “Mwenyezi-Mungu ataniokoa. Nasi tutamsifu kwa nyimbo za vinubi siku zote za maisha yetu, nyumbani kwake Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 “Mwenyezi-Mungu ataniokoa. Nasi tutamsifu kwa nyimbo za vinubi siku zote za maisha yetu, nyumbani kwake Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Mwenyezi Mungu ataniokoa, nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi siku zote za maisha yetu katika Hekalu la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 bwana ataniokoa, nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi siku zote za maisha yetu katika Hekalu la bwana.

Tazama sura Nakili




Isaya 38:20
19 Marejeleo ya Msalaba  

Nitamwimbia BWANA maadamu ninaishi; Nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai;


Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.


Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.


Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele.


Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.


Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;


Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.


Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.


Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.


Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu.


Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari.


Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.


BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona katika pwani.


MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo