Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 36:7 - Swahili Revised Union Version

7 Lakini ukiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini hata kama mkiniambia, ‘Tunamtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,’ je, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu madhabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuabudu mbele ya madhabahu hii?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini hata kama mkiniambia, ‘Tunamtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,’ je, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu madhabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuabudu mbele ya madhabahu hii?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini hata kama mkiniambia, ‘Tunamtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu,’ je, si huyohuyo ambaye Hezekia aliziharibu madhabahu zake na kuwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuabudu mbele ya madhabahu hii?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nawe ukiniambia, “Tunamtumainia Mwenyezi Mungu, Mungu wetu”: Je, si yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nawe kama ukiniambia, “Tunamtumainia bwana Mwenyezi Mungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Lakini ukiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu, je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake mlimoinuka, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii?

Tazama sura Nakili

Isaya 36:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mkiniambia, Tunamtumaini BWANA, Mungu wetu; je! Si yeye ambaye Hezekia ameondoa mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, Sujuduni mbele ya madhabahu hii hapa Yerusalemu?

Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.

Wakainuka, wakaziondoa madhabahu zilizokuwamo Yerusalemu, nazo madhabahu za kufukizia wakaziondoa, wakazitupa katika kijito Kidroni.

Basi hayo yote yalipokwisha, Israeli wote waliokuwako wakatoka waende miji ya Yuda, wakazivunjavunja nguzo, wakayakatakata Maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hadi walipoviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao.

Si yeye Hezekia huyo aliyeondoa mahali pake pa juu, na madhabahu zake, akawaamuru Yuda na Yerusalemu, akisema, Abuduni mbele ya madhabahu moja, na juu yake mtafukiza uvumba?

Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.

Basi sasa, tafadhali mpe bwana wangu, mfalme wa Ashuru, dhamana, nami nitakupa farasi elfu mbili, ikiwa wewe kwa upande wako waweza kupandisha watu juu yao.

Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo