Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 34:16 - Swahili Revised Union Version

16 Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu: “Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwako na mwenzake.” Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo, roho yake itawakusanya hao wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu: “Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwako na mwenzake.” Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo, roho yake itawakusanya hao wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Someni katika kitabu cha Mwenyezi-Mungu: “Hakuna hata kiumbe kimoja kitakachokosekana, kila kimoja kitakuwako na mwenzake.” Maana Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hivyo, roho yake itawakusanya hao wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Angalieni katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na msome: Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake Mtakatifu atawakusanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Angalieni katika gombo la bwana na msome: Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana, hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake. Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza, na Roho wake atawakusanya pamoja.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.

Tazama sura Nakili




Isaya 34:16
22 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.


Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.


Maana Yeye alisema, na ikawa; Na Yeye aliamuru, ikaumbika.


Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.


bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.


Piga yowe, Ee lango; lia, Ee mji; Ee Ufilisti enyi wote, umeyeyuka kabisa; Maana moshi unakuja toka kaskazini, Wala hakuna atakayechelewa katika majeshi yake.


Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana BWANA, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.


Haya, nenda sasa, andika neno hili katika kibao mbele ya macho yao, lichore katika kitabu ili liwe kwa ajili ya majira yatakayokuja, kwa ushuhuda hata milele.


Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.


Na utukufu wa BWANA utafunuliwa, Na watu wote watauona pamoja; Kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.


ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.


Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.


Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.


Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.


Ndipo wale waliomcha BWANA waliposemezana wao kwa wao. Naye BWANA akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha BWANA, na kulitafakari jina lake.


Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.


Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.


Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);


Mnayachunguza maandiko kwa sababu mnadhani kuwa ndani yake ninyi mna uzima wa milele; na maandiko yayo hayo ndiyo yanayonishuhudia.


Tena itakuwa, wakiisha kujiliwa na mambo maovu mengi na mashaka, utashuhudia wimbo huu mbele yao kama shahidi, kwa maana hautasahauliwa katika vinywa vya uzao wao; kwani nayajua mawazo yao wayawazayo, hata sasa kabla sijawatia katika nchi niliyoapa.


Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo