Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 27:7 - Swahili Revised Union Version

7 Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mungu hakuwaadhibu Waisraeli vikali kama alivyowaadhibu maadui wake; Waisraeli waliopotea vitani, ni wachache kuliko wale wa maadui zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mungu hakuwaadhibu Waisraeli vikali kama alivyowaadhibu maadui wake; Waisraeli waliopotea vitani, ni wachache kuliko wale wa maadui zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mungu hakuwaadhibu Waisraeli vikali kama alivyowaadhibu maadui wake; Waisraeli waliopotea vitani, ni wachache kuliko wale wa maadui zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Je, Mwenyezi Mungu amempiga vile alivyowapiga wale waliompiga? Je, yeye ameuawa vile walivyouawa wale waliomuua yeye?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Je, bwana amempiga vile alivyowapiga wale waliompiga? Je, yeye ameuawa vile walivyouawa wale waliomuua yeye?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?

Tazama sura Nakili




Isaya 27:7
17 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitamwadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.


Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa muali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake kwa siku moja.


Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang'anya mali zetu.


Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.


Maana kwa sauti ya BWANA, Mwashuri atavunjikavunjika, yeye apigaye kwa bakora.


Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.


Na mwamba wake utatoweka kwa sababu ya hofu, nao wakuu wake wataionea bendera hofu kuu, asema BWANA, ambaye moto wake u katika Sayuni, na tanuri yake katika Yerusalemu.


Kama vile ilivyotokea Mungu alipoangusha Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; kadhalika hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama wageni wakaavyo.


Nami nitamlipa Babeli, na wote wakaao ndani ya Ukaldayo, mabaya yao yote, waliyoyatenda katika Sayuni mbele ya macho yenu, asema BWANA.


Tena BWANA ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asiwepo tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.


Jeraha lako halipunguziki; donda lako haliponyeki; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani aliyewahi kuukwepa ukatili wako usio na mwisho?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo