Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 19:11 - Swahili Revised Union Version

11 Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmoja wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?

Tazama sura Nakili




Isaya 19:11
31 Marejeleo ya Msalaba  

Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya watu wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.


Basi Hiramu akampa Sulemani miti ya mierezi na miti ya miberoshi kadiri alivyotaka.


Yeye huwaondoa washauri wakiwa wamevuliwa nguo, Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.


BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huitangua mipango ya watu.


Nilikuwa kama mjinga, sijui neno; Nilikuwa kama mnyama tu mbele zako.


Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu, Katika nchi ya Misri, konde la Soani.


Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika uwanda wa Soani.


Mtu mjinga hayatambui hayo, Wala mpumbavu hayafahamu.


Wakawakusanya marundo marundo; na nchi ikatoa uvundo.


Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote.


Hakika nimekuwa kama mnyama, wala si mtu; Wala sina ufahamu wa mwanadamu;


Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu, wakuu wa Nofu wamedanganyika; na hao walio mawe ya pembeni ya kabila zake wameipotosha Misri.


Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi.


kwa sababu hiyo mimi nitafanya tena kazi ya ajabu kati ya watu hawa, kazi ya ajabu na mwujiza; na akili za watu wao wenye akili zitapotea, na ufahamu wa wenye busara wao utafichwa.


Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi.


Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;


Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga; Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo, Wala hamna pumzi ndani yake.


Kwa sababu wachungaji wamekuwa kama wanyama, wala hawakuuliza kwa BWANA; basi hawakufanikiwa, na makundi yao yote yametawanyika.


Wakalia huko, Farao, mfalme wa Misri, ni kishindo tu; muda alioandikiwa ameuacha upite.


Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?


Wenye hekima wametahayari, wamefadhaika na kushikwa; tazama, wamelikataa neno la BWANA, wana akili gani ndani yao?


Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.


Nami nitaifanya Pathrosi kuwa ukiwa, nami nitatia moto katika Soani, nami nitatekeleza hukumu katika No.


Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari; nao watakwenda kwa nabii kutaka maono; lakini hiyo sheria itampotea kuhani, na mashauri yatawapotea wazee.


Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hadi mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.


Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema BWANA.


Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.


Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo