Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 18:5 - Swahili Revised Union Version

5 Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua umekwisha, maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu, Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea, na kuyakwanyua matawi yanayotanda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua umekwisha, maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu, Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea, na kuyakwanyua matawi yanayotanda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua umekwisha, maua yamepukutika na kuwa zabibu mbivu, Mungu atakata chipukizi kwa kisu cha kupogolea, na kuyakwanyua matawi yanayotanda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Kwa maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua ukishapita na maua yakawa zabibu zinazoiva, atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi, naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Kwa maana, kabla ya mavuno, wakati wa kuchanua ukishapita na maua yakawa zabibu zinazoiva, atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi, naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata.

Tazama sura Nakili

Isaya 18:5
6 Marejeleo ya Msalaba  

Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako.

Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.

Angalia, Bwana, BWANA wa majeshi, atayakata matawi kwa nguvu za kutisha; nao walio warefu wa kimo watakatwa; na hao walioinuka wataangushwa chini;

Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo