Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 14:2 - Swahili Revised Union Version

2 Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Mwenyezi Mungu. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kuwatawala waliowadhulumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya bwana. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kutawala juu ya wale waliowaonea.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea.

Tazama sura Nakili




Isaya 14:2
34 Marejeleo ya Msalaba  

tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.


Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, BWANA Mungu akae nao.


Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hidaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inagawanya nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.


Ndipo huyo Mwashuri ataanguka kwa upanga ambao si wa mtu; na upanga usio upanga wa mtu utamwangamiza; naye ataukimbia upanga, na vijana wake watatoa kodi.


BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.


Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwainulia makabila ya watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.


Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.


Naam, BWANA asema hivi, Hata mateka wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka wake aliye katili wataokoka; kwa maana nitapambana na yeye abishanaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.


Kwa maana utaenea upande wa kulia na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.


Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.


Inua macho yako, utazame pande zote; Wote wanakusanyana; wanakujia wewe; Wana wako watakuja kutoka mbali. Na binti zako watabebwa nyongani.


Na wageni watasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabila nyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wa mizabibu yenu.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo.


Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya kishindo cha vita kisikike juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema BWANA.


hata hawataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao watawateka nyara watu waliowateka wao, na kuwapora watu waliowapora wao, asema Bwana MUNGU.


Lakini watakatifu wake Aliye Juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele.


Na mimi nitawauza wana wenu na binti zenu, na kuwatia katika mikono ya wana wa Yuda, nao watawauzia watu wa Sheba, taifa lililo mbali kabisa; kwa maana BWANA ndiye aliyesema neno hili.


Tena kuhusu watumishi wako na wajakazi wako, utakaokuwa nao; mataifa walio kando yenu, katika hao mtanunua watumishi na wajakazi.


Bali katika mlima Sayuni kutakuwa na watakaookoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki tena milki zao.


Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.


Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma.


Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga watumwa wenzake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;


Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumia kwa mambo yao ya mwili.


tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.


Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.


Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo