Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 13:8 - Swahili Revised Union Version

8 Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watagaagaa kama mwanamke aliye na uchungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwaka kama moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwaka kama moto.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.

Tazama sura Nakili




Isaya 13:8
21 Marejeleo ya Msalaba  

Ndiyo sababu wenyeji wao walikuwa na nguvu chache, wakafadhaika, na kuhangaika; wakawa kama majani ya mashamba, kama miche mibichi, kama majani juu ya dari, na kama ngano iliyokaushwa kabla haijaiva.


Kama upepo wa mashariki Unapovunja jahazi za Tarshishi.


Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na uchungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee BWANA.


Utasema nini wewe, atakapowaweka rafiki zako kuwa kichwa juu yako, ikiwa wewe mwenyewe umewafundisha kuwa juu yako? Je! Huzuni haitakushika, kama uchungu wa mwanamke aliye katika kuzaa?


Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona uchungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na uchungu, na nyuso zote zimegeuka rangi?


Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.


Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.


Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemeko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika uchungu wake.


Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana; Wanakaa katika ngome zao; Ushujaa wao umewapungukia; Wamekuwa kama wanawake; Makao yake yameteketea; Makomeo yake yamevunjika.


ukauambie msitu wa Negebu, Lisikie neno la BWANA; Bwana MUNGU asema hivi; Tazama nitawasha moto ndani yako, nao utakula kila mti mbichi ndani yako, na kila mti mkavu; miali ya moto ule haitazimika, na nyuso zote toka kusini hadi kaskazini zitateketezwa kwa moto huo.


Uchungu wa mwanamke mwenye mimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili; maana wakati umewadia, ambao haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto.


Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu.


Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagonganagongana; moyoni kote mna uchungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.


Mwanamke azaapo, ana huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni.


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo