Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 7:1 - Swahili Revised Union Version

1 Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwizi huvunja nyumba za watu, na kundi la magaidi hushambulia nje.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kila nikitaka kuwarekebisha watu wangu, ninapotaka kuwaponya Waisraeli, uovu wa watu wa Efraimu hufunuliwa, matendo mabaya ya Samaria hujitokeza. Wao huongozwa na udanganyifu, kwenye nyumba wezi huvunja nje barabarani wanyang'anyi huvamia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wezi huvunja nyumba, maharamia hunyang’anya barabarani,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 kila mara nilipotaka kumponya Israeli, dhambi za Efraimu zinafichuliwa na maovu ya Samaria yanafunuliwa. Wanafanya udanganyifu, wevi huvunja nyumba, maharamia hunyang’anya barabarani,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Wakati nitakapo kumponya Israeli, ndipo yafunuliwapo maovu ya Efraimu, na ubaya wa Samaria; maana wanatenda uongo, na mwizi huvunja nyumba za watu, na kundi la wanyang'anyi hushambulia nje.

Tazama sura Nakili




Hosea 7:1
30 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wa taji la kiburi la walevi wa Efraimu, na ua la uzuri wa fahari yake linalonyauka, lililo kichwani mwa bonde linalositawi, la hao walioshindwa na divai!


Maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi, na maovu yetu tumeyajua;


katika kukosa na kumkana BWANA, na katika kugeuka tusimfuate Mungu wetu, tukinena udhalimu na uasi, na kukusudia maneno ya uongo na kuyatoa moyoni.


Na hukumu imegeuka ikaenda nyuma, na haki inasimama mbali sana; maana kweli imeanguka katika njia kuu, na unyofu hauwezi kuingia.


Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.


Na dada yako mkubwa ni Samaria, akaaye mkono wako wa kushoto, yeye na binti zake; na dada yako mdogo, akaaye mkono wako wa kulia, ni Sodoma na binti zake.


Na majina yao, mkubwa aliitwa Ohola, na dada yake Oholiba; wakawa wangu, wakazaa watoto wa kiume na wa kike. Na katika hayo majina yao, Samaria ni Ohola, na Yerusalemu ni Oholiba.


Katika uchafu wako mna uasherati, kwa maana nimekusafisha, ila wewe hukusafika; hutasafishwa tena uchafu wako ukutoke, hadi nitakapokuwa nimeituliza hasira yangu kwako.


Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.


Efraimu amenizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu; na Yuda hata sasa anasitasita kwa Mungu, na kwake aliye Mtakatifu, naye ni mwaminifu.


Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.


Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.


BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.


Efraimu amejiungamanisha na sanamu; mwache.


Hapana neno ila kuapa kwa uongo, na kuvunja ahadi, na kuua, na kuiba, na kuzini; huruka mpaka, na kumwaga damu mfululizo.


Sikieni haya, enyi makuhani, sikilizeni, enyi nyumba ya Israeli, tegeni masikio yenu, enyi wa nyumba ya mfalme, kwa kuwa hukumu hii yawahusu ninyi; maana mmekuwa mtego huko Mizpa, na wavu uliotandwa juu ya Tabori.


Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao mapema.


Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.


Ndama wako amemtupa, Ee Samaria; ghadhabu yangu imewaka juu yao; Wataendelea kuwa na hatia hadi lini?


Kwa maana wamekwea kwenda Ashuru, mfano wa punda wa porini aliye peke yake; Efraimu ameajiri wapenzi.


Kwa maana hawajui kutenda haki, asema BWANA, hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.


Tangazeni habari katika majumba ya Ashdodi, na katika majumba ya nchi ya Misri, mkaseme, Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria, katazameni, ni mishindo mikubwa kama nini iliyomo humo, na udhalimu mwingi kama nini uliomo ndani yake.


Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.


Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.


Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!


Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii na kuwapiga kwa mawe waliotumwa kwako, mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mbawa zake, wala hamkutaka.


akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo