Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 10:1 - Swahili Revised Union Version

1 Israeli ni mzabibu mzuri, utoao matunda yake; kwa kadiri ya wingi wa matunda yake, kwa kadiri iyo hiyo ameongeza madhabahu zake; kwa kadiri ya wema wa nchi yake, kwa kadiri iyo hiyo wamefanya nguzo nzuri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Waisraeli walikuwa kama mzabibu mzuri, mzabibu wenye kuzaa matunda. Kadiri matunda yalivyozidi kuongezeka, ndivyo walivyozidi kujijengea madhabahu. Kadiri nchi yao ilivyozidi kustawi, ndivyo walivyozidi kupamba nguzo zao za ibada.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana, alijizalia matunda mwenyewe. Kadiri matunda yake yalivyoongezeka, alijenga madhabahu zaidi; kadiri nchi yake ilivyostawi, alipamba mawe yake ya ibada.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Israeli ni mzabibu mzuri, utoao matunda yake; kwa kadiri ya wingi wa matunda yake, kwa kadiri hiyo hiyo ameongeza madhabahu zake; kwa kadiri ya wema wa nchi yake, kwa kadiri hiyo hiyo wamefanya nguzo nzuri.

Tazama sura Nakili




Hosea 10:1
24 Marejeleo ya Msalaba  

Maana hao pia wakajijengea mahali pa juu, na nguzo, na maashera, juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.


Maana hesabu ya miungu yako, Ee Yuda, ni sawasawa na hesabu ya miji yako; na kama ilivyo hesabu ya njia za Yerusalemu, ndivyo mlivyosimamisha madhabahu za kitu kile cha aibu, madhabahu za kumfukizia Baali uvumba.


Kwa maana BWANA wa majeshi, aliyekupanda, ametamka mabaya juu yako, kwa sababu ya maovu ya nyumba ya Israeli, na ya nyumba ya Yuda, waliyoyatenda juu ya nafsi zao wenyewe kwa kunikasirisha, wakimfukizia Baali uvumba.


Lakini wako wapi miungu yako ulioifanya? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.


Katika Gileadi kuna uovu? Nao wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng'ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.


Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wowote uliokuwa dhambi.


Ajapokuwa yeye ni mwenye kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya BWANA itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.


Na sasa wanazidi kufanya dhambi, nao wamejifanyia sanamu kwa fedha yao, naam, sanamu kwa kadiri ya akili zao; zote pia ni kazi ya mafundi; nao huzitaja hivi, Wanaume watoao dhabihu na wazibusu ndama.


Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau mimi.


Na sasa nitaifunua aibu yake mbele ya macho ya wapenzi wake, wala hapana mtu atakayemwokoa katika mkono wangu.


Maana hakujua ya kuwa mimi ndiye niliyempa ngano, na divai, na mafuta, na kumwongezea fedha na dhahabu, walivyovitumia kwa ajili ya Baali.


Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;


Kadiri walivyozidishwa, kwa kadiri iyo hiyo walinitenda dhambi; nami nitageuza utukufu wao kuwa aibu.


Kwa kuwa Efraimu ameongeza madhabahu kwa dhambi, madhabahu zimekuwa dhambi kwake.


Wamesimamisha wafalme, lakini si kwa shauri langu; wamejifanyia wakuu, lakini nilikuwa sina habari; kwa fedha yao na dhahabu yao wamejifanyia sanamu, kusudi wakatiliwe mbali.


Msifanye sanamu yoyote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lolote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


Kwa maana BWANA anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.


Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.


Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo