Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 1:2 - Swahili Revised Union Version

2 Hapo kwanza BWANA aliponena kwa kinywa cha Hosea, BWANA alimwambia Hosea, Nenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Mwenyezi-Mungu alipoanza kuongea na Waisraeli kwa njia ya Hosea, alimwambia hivi: “Nenda ukaoe mwanamke mzinzi, uzae naye watoto wa uzinzi, maana watu wa nchi hii wanafanya uzinzi mwingi kwa kuniacha mimi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Mwenyezi-Mungu alipoanza kuongea na Waisraeli kwa njia ya Hosea, alimwambia hivi: “Nenda ukaoe mwanamke mzinzi, uzae naye watoto wa uzinzi, maana watu wa nchi hii wanafanya uzinzi mwingi kwa kuniacha mimi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Mwenyezi-Mungu alipoanza kuongea na Waisraeli kwa njia ya Hosea, alimwambia hivi: “Nenda ukaoe mwanamke mzinzi, uzae naye watoto wa uzinzi, maana watu wa nchi hii wanafanya uzinzi mwingi kwa kuniacha mimi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mwenyezi Mungu alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, Mwenyezi Mungu alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wakati bwana alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, bwana alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha bwana.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Hapo kwanza BWANA aliponena kwa kinywa cha Hosea, BWANA alimwambia Hosea, Nenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha BWANA.

Tazama sura Nakili




Hosea 1:2
24 Marejeleo ya Msalaba  

lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaongoza Yuda na wakazi wa Yerusalemu kwenye kukosa uaminifu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe;


Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, Wakafanya uasherati kwa matendo yao.


Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe.


Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.


Kwa maana tangu zamani wewe umeivunja nira yako, na kuvipasua vifungo vyako; ukasema, Mimi sitatumika; kwa maana juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, umejiinamisha, ukafanya mambo ya ukahaba.


Wawezaje kusema, Sikutiwa unajisi, sikuwafuata Mabaali? Itazame njia yako bondeni, ujue uliyoyatenda; wewe u ngamia mwepesi, apitaye katika njia zake;


Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti.


Na hao wa kwenu watakaookoka watanikumbuka kati ya mataifa, watakakochukuliwa mateka, jinsi nilivyoiponda mioyo yao ya kikahaba, iliyoniacha, na macho yao, yaendayo kufanya uasherati na vinyago vyao; nao watajichukia nafsi zao machoni pao wenyewe, kwa sababu ya mabaya yao yote, waliyoyatenda kwa machukizo yao yote.


Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.


BWANA akaniambia, Nenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile BWANA awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.


Mimi namjua Efraimu, wala Israeli hakufichwa nisimwone; maana sasa, Ee Efraimu, umefanya uzinzi; Israeli ametiwa unajisi.


Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.


BWANA akamwambia Musa, Angalia, wewe utalala na baba zako; na watu hawa wataondoka, wataifuata kwa ukahaba miungu ya kigeni ya nchi waiendeayo kuwa kati yao, nao wataniacha mimi na kulivunja agano langu, nililofanya nao.


wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;


Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, Babeli MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo