Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 7:88 - Swahili Revised Union Version

88 na ng'ombe wote waliokuwa wa dhabihu ya sadaka za amani ni ng'ombe dume ishirini na wanne, na hao kondoo dume walikuwa ni sitini, na hao mbuzi dume walikuwa ni sitini, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa sitini. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, baada ya hiyo madhabahu kutiwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

88 na kwa ajili ya tambiko ya sadaka ya amani, jumla ya wanyama waliotolewa ilikuwa mafahali ishirini na wanne, kondoo madume sitini, beberu sitini, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja sitini. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka iliyotolewa kwa ajili ya madhabahu, baada ya madhabahu hiyo kupakwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

88 na kwa ajili ya tambiko ya sadaka ya amani, jumla ya wanyama waliotolewa ilikuwa mafahali ishirini na wanne, kondoo madume sitini, beberu sitini, na wanakondoo madume wa mwaka mmoja sitini. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka iliyotolewa kwa ajili ya madhabahu, baada ya madhabahu hiyo kupakwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

88 Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo dume sitini, beberu wa mwaka mmoja sitini, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja sitini. Hizo ndizo sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kupakwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

88 Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo dume sitini, mbuzi dume wa mwaka mmoja sitini na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja sitini. Hizi ndizo zilikuwa sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

88 na ng'ombe wote waliokuwa wa dhabihu ya sadaka za amani ni ng'ombe dume ishirini na wanne, na hao kondoo dume walikuwa ni sitini, na hao mbuzi dume walikuwa ni sitini, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa sitini. Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, baada ya hiyo madhabahu kutiwa mafuta.

Tazama sura Nakili

Hesabu 7:88
5 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani dhabihu kwa BWANA, itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yake, na mkia wenye mafuta mzima, atauondoa kwa kuukata hapo karibu na mfupa wa maungoni; na mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo katika matumbo,

Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa;

Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu.

Hayo ndiyo matoleo yaliyotolewa na wakuu wa Israeli kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, siku hiyo ilipotiwa mafuta; sahani za fedha kumi na mbili, na bakuli za fedha kumi na mbili, na vijiko vya dhahabu kumi na viwili;

ng'ombe wote waliokuwa wa sadaka ya kuteketezwa walikuwa ng'ombe dume kumi na wawili, na hao kondoo dume walikuwa kumi na wawili, na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja walikuwa kumi na wawili, pamoja na sadaka yao ya unga; na mbuzi dume wa sadaka ya dhambi ni kumi na wawili;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo