Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 6:12 - Swahili Revised Union Version

12 Kisha ataziweka kwa BWANA hizo siku za kujitenga kwake, naye ataleta mwana-kondoo wa kiume wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya hatia; lakini hizo siku za kwanza hazitahesabiwa, kwa kuwa kule kujitenga kwake kulitiwa unajisi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 na kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa siku zake za kujitenga. Hizo siku za kwanza hazitahesabiwa kwa sababu nywele zake zilizokuwa zimewekwa wakfu zimetiwa unajisi. Atatoa mwanakondoo dume wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 na kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa siku zake za kujitenga. Hizo siku za kwanza hazitahesabiwa kwa sababu nywele zake zilizokuwa zimewekwa wakfu zimetiwa unajisi. Atatoa mwanakondoo dume wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya hatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 na kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu kwa siku zake za kujitenga. Hizo siku za kwanza hazitahesabiwa kwa sababu nywele zake zilizokuwa zimewekwa wakfu zimetiwa unajisi. Atatoa mwanakondoo dume wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Ni lazima ajitoe kabisa kwa Mwenyezi Mungu kwa kipindi cha kujitenga kwake, na ni lazima atoe mwana-kondoo wa kiume wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya hatia. Siku zilizopita hazitahesabiwa kwa sababu alijitia unajisi katika siku zake za kujitenga.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Ni lazima ajitoe kabisa kwa bwana kwa kipindi cha kujitenga kwake, na ni lazima atoe mwana-kondoo wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Siku zilizopita hazitahesabiwa kwa sababu alijitia unajisi katika siku zake za kujitenga.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Kisha ataziweka kwa BWANA hizo siku za kujitenga kwake, naye ataleta mwana-kondoo dume wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya hatia; lakini hizo siku za kwanza hazitahesabiwa, kwa kuwa kule kujitenga kwake kulitiwa unajisi.

Tazama sura Nakili




Hesabu 6:12
12 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana-kondoo wenu atakuwa hana dosari, wa kiume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.


Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.


Na kuhani atamtwaa huyo mwana-kondoo wa sadaka ya hatia, na hiyo logi ya mafuta, naye kuhani atavitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA;


naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.


Lakini asipomweza mwana-kondoo, ndipo atakapomletea BWANA hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, kuwa ni sadaka yake ya hatia ya jambo hilo alilolikosa; mmoja wa hao ndege kwa sadaka ya dhambi, na wa pili kwa sadaka ya kuteketezwa.


naye kuhani atasongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa, naye atafanya upatanisho kwa ajili yake, kwa sababu aliingia kosani kwa ajili ya maiti, naye atatakasa kichwa chake siku iyo hiyo.


Na sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa mlangoni pa hema ya kukutania;


Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.


Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali.


Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.


Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo