Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 36:13 - Swahili Revised Union Version

13 Haya ndiyo maagizo na hukumu, ambayo BWANA aliwaagiza wana wa Israeli, kwa mkono wa Musa, hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hizo ndizo amri na maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli kwa njia ya Mose katika tambarare za Moabu, ngambo ya Mto Yordani karibu na mji wa Yeriko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hizo ndizo amri na maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli kwa njia ya Mose katika tambarare za Moabu, ngambo ya Mto Yordani karibu na mji wa Yeriko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hizo ndizo amri na maagizo ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli kwa njia ya Mose katika tambarare za Moabu, ng'ambo ya Mto Yordani karibu na mji wa Yeriko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Haya ndio maagizo na masharti ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa Waisraeli kupitia Musa katika tambarare za Moabu, karibu na Yordani ng’ambo ya Yeriko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Haya ndiyo maagizo na masharti ambayo bwana aliwapa Waisraeli kupitia Musa katika tambarare za Moabu, karibu na Yordani ng’ambo ya Yeriko.

Tazama sura Nakili




Hesabu 36:13
12 Marejeleo ya Msalaba  

Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi;


Na katika pigo la ukoma katika vazi la sufu, au la kitani, kama ni katika lililofumwa, au lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, sheria yake ni hiyo, kusema kwamba ni safi, au kusema kwamba ni najisi.


Hizi ni amri, maagizo na sheria, BWANA alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.


Haya ndiyo maagizo, BWANA aliyomwagiza Musa kwa ajili ya wana wa Israeli katika mlima wa Sinai.


Kisha wana wa Israeli wakasafiri na kupanga katika nchi tambarare za Moabu ng'ambo ya pili ya Yordani karibu na Yeriko.


Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia,


Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia,


Kisha BWANA akanena na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko, akamwambia,


Waliolewa katika jamaa za wana wa Manase, mwana wa Yusufu, na urithi wao ukakaa katika kabila la jamaa ya baba yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo