Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 35:2 - Swahili Revised Union Version

2 Uwaagize wana wa Israeli wawape Walawi miji wapate mahali pa kukaa, katika milki yao; pamoja na malisho yaliyoizunguka hiyo miji kotekote mtawapa Walawi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Waamuru Waisraeli kwamba kutokana na urithi watakaomiliki, wawape Walawi miji ya kukaa na sehemu za malisho kandokando ya miji hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Waamuru Waisraeli kwamba kutokana na urithi watakaomiliki, wawape Walawi miji ya kukaa na sehemu za malisho kandokando ya miji hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Waamuru Waisraeli kwamba kutokana na urithi watakaomiliki, wawape Walawi miji ya kukaa na sehemu za malisho kandokando ya miji hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Waagize Waisraeli kuwapa Walawi miji ya kuishi kutoka urithi ambao Waisraeli wataumiliki. Wape maeneo ya malisho kuzunguka hiyo miji.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Waagize Waisraeli kuwapa Walawi miji ya kuishi kutoka urithi ambao Waisraeli wataumiliki. Wape maeneo ya malisho kuzunguka hiyo miji.

Tazama sura Nakili




Hesabu 35:2
14 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa BWANA, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;


Walawi wakaacha malisho yao, na milki yao, wakaja Yuda na Yerusalemu; kwa sababu Yeroboamu na wanawe waliwakataza, ili wasimfanyie BWANA ukuhani;


tena kwa ajili ya wana wa Haruni makuhani, waliokuwamo mashambani mwa malisho ya miji yao, mji kwa mji, kulikuwa na watu waliotajwa majina yao, ili kuwagawia sehemu wanaume wote miongoni mwa makuhani, na wote waliohesabiwa kwa nasaba miongoni mwa Walawi.


Tena nikagundua kwamba Walawi hawakupewa sehemu zao; Hivyo Walawi na waimbaji walioongoza ibada, kila mtu amerudi shambani mwake.


Tena tokea milki ya Walawi, na tokea milki ya mji, kwa kuwa ni katikati ya nchi iliyo ya mkuu, katikati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini, itakuwa ya mkuu.


Na mpakani mwa Yuda, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi, yatakuwapo matoleo mtakayotoa, upana wake mianzi elfu ishirini na tano, na urefu wake sawasawa na moja la mafungu hayo, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; na mahali patakatifu ni katikati yake.


Kisha BWANA akanena na Musa katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko, akamwambia,


Hiyo miji watakuwa nayo ili wakae humo, na malisho watakuwa nayo kwa wanyama wao wa mifugo, na kwa mali zao, na kwa wanyama wao wote.


Na akija Mlawi atokaye katika malango yako mojawapo, katika Israeli yote alipokuwa akikaa, akaja kwa mapenzi yote ya nafsi yake mahali atakapochagua BWANA;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo