Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 32:4 - Swahili Revised Union Version

4 nchi hiyo ambayo BWANA aliipiga mbele ya mkutano wa Israeli, ni nchi ifaayo kwa mifugo, nasi watumishi wako tunayo mifugo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 nchi ambayo Mwenyezi-Mungu alishinda kwa ajili ya jumuiya ya Israeli, ni nchi nzuri kwa mifugo, nasi tunayo mifugo mingi sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 nchi ambayo Mwenyezi-Mungu alishinda kwa ajili ya jumuiya ya Israeli, ni nchi nzuri kwa mifugo, nasi tunayo mifugo mingi sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 nchi ambayo Mwenyezi-Mungu alishinda kwa ajili ya jumuiya ya Israeli, ni nchi nzuri kwa mifugo, nasi tunayo mifugo mingi sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 nchi ambayo Mwenyezi Mungu ameishinda mbele ya Waisraeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 nchi ambayo bwana ameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 nchi hiyo ambayo BWANA aliipiga mbele ya mkutano wa Israeli, ni nchi ifaayo kwa mifugo, nasi watumishi wako tunayo mifugo.

Tazama sura Nakili




Hesabu 32:4
9 Marejeleo ya Msalaba  

Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuziharibu hema zao, pamoja na hao Wameuni waliokuwa wakiishi huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo wao.


Nami nitamleta Israeli tena malishoni kwake, naye atalisha juu ya Karmeli, na Bashani, na nafsi yake itashiba juu ya milima ya Efraimu, na katika Gileadi.


Walishe watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako, wakaao peke yao, msituni katikati ya Karmeli; na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.


Israeli wakampiga kwa makali ya upanga, na kuimiliki nchi yake, tangu mto wa Arnoni hata mto wa Yaboki, mpaka nchi ya wana wa Amoni; kwa kuwa mpaka wa wana wa Amoni ulikuwa una nguvu.


BWANA akamwambia Musa, Usimche; kwa kuwa nimekwisha mtia mkononi mwako, na watu wake wote, na nchi yake; nawe utamtenda kama ulivyomtenda Sihoni mfalme wa Waamori, aliyeishi Heshboni.


Basi wakampiga, na wanawe, na watu wake wote, hata wasibakize kwake mtu yeyote; nao wakaimiliki nchi yake.


Wakasema, Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, sisi watumishi wako na tupewe nchi hii iwe milki yetu; usituvushe mto wa Yordani.


ili kufukuza mbele yako mataifa, walio wakubwa, wenye nguvu kukupita wewe, ili kukuingiza, na kukupa nchi yao iwe urithi, kama ilivyo leo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo