Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 32:13 - Swahili Revised Union Version

13 Na hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huko jangwani muda wa miaka arubaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa BWANA kilipoisha angamia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mwenyezi-Mungu aliwaka hasira dhidi ya Waisraeli, akawafanya watangetange jangwani kwa muda wa miaka arubaini; kizazi kizima kilichokuwa kimefanya maovu mbele yake kikafariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mwenyezi-Mungu aliwaka hasira dhidi ya Waisraeli, akawafanya watangetange jangwani kwa muda wa miaka arubaini; kizazi kizima kilichokuwa kimefanya maovu mbele yake kikafariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mwenyezi-Mungu aliwaka hasira dhidi ya Waisraeli, akawafanya watangetange jangwani kwa muda wa miaka arubaini; kizazi kizima kilichokuwa kimefanya maovu mbele yake kikafariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Hasira ya Mwenyezi Mungu iliwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, hadi kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Hasira ya bwana iliwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, mpaka kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Na hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huko jangwani muda wa miaka arobaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa BWANA kilipoisha angamia.

Tazama sura Nakili




Hesabu 32:13
15 Marejeleo ya Msalaba  

Walitangatanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa.


Kwa hiyo akazikomesha siku zao kama pumzi, Na miaka yao kwa hofu ya kuwastusha.


Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile, Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka, Na wanaopuuza njia zangu.


Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arubaini, hata walipofikia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikia mipakani mwa nchi ya Kanaani.


Pia niliwapandisha ninyi kutoka nchi ya Misri, nikawaongoza muda wa miaka arubaini jangwani, ili mpate kuimiliki nchi ya Mwamori.


Lakini nilimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini niliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.


Lakini katika habari zenu, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili.


Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.


Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubariki katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arubaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.


Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akawatia katika mikono ya watu waliowateka nyara, akawauza na kuwatia katika mikono ya adui zao pande zote; hata wasiweze tena kusimama mbele ya adui zao.


Basi hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili limelivunja agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo