Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 28:3 - Swahili Revised Union Version

3 Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsogezea BWANA; wana-kondoo dume wawili wa mwaka mmoja wakamilifu, kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Waambie kwamba sadaka watakayonitolea ya kuteketezwa kwa moto, itakuwa ifuatavyo: Wanakondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari yoyote, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Waambie kwamba sadaka watakayonitolea ya kuteketezwa kwa moto, itakuwa ifuatavyo: Wanakondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari yoyote, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Waambie kwamba sadaka watakayonitolea ya kuteketezwa kwa moto, itakuwa ifuatavyo: wanakondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari yoyote, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Mwenyezi Mungu: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kuwa sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsogezea BWANA; wana-kondoo dume wawili wa mwaka mmoja wakamilifu, kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya siku zote.

Tazama sura Nakili




Hesabu 28:3
25 Marejeleo ya Msalaba  

ili kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa daima asubuhi na jioni, naam, kulingana na yote yaliyoandikwa katika Torati ya BWANA, aliyowaamuru Israeli;


kadiri ilivyohitajiwa huduma ya kila siku, akitoa sawasawa na amri ya Musa, siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoamriwa, mara tatu kila mwaka, yaani, sikukuu ya mikate isiyochachwa, na sikukuu ya majuma, na sikukuu ya vibanda.


na baadaye sadaka ya kuteketezwa ya daima, na za mwandamo wa mwezi, na za sikukuu za BWANA, zilizoamriwa na kuwekwa wakfu, na za kila mtu aliyemtolea BWANA sadaka kwa hiari yake.


Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.


Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itaondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na tisini.


Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.


Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono kuhusu habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa liletalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyaga patakatifu na jeshi?


Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa BWANA.


Haya, mwagize Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya sadaka ya kuteketezwa ni hii; hiyo sadaka ya kuteketezwa itakuwa pale motoni juu ya madhabahu usiku wote hadi asubuhi; na huo moto wa madhabahu utawaka juu yake usizimike.


Njooni Betheli, mkakose; njoni Gilgali, mkaongeze makosa; kaleteni dhabihu zenu kila asubuhi, na zaka zenu kila siku ya tatu;


hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila Sabato, zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.


Tena mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.


Mtasongeza wanyama hao zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, iliyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote.


Mtasongeza sadaka kwa jinsi hii kila siku kwa muda wa siku saba, chakula cha sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa BWANA; itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.


Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.


Mwana-kondoo mmoja utamsongeza asubuhi, na mwana-kondoo wa pili utamsongeza jioni;


na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; zaidi ya hiyo sadaka ya dhambi ya upatanisho, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.


na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.


zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya kuandama mwezi, na sadaka yake ya unga, na hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji, kama ilivyo amri yake, kuwa harufu ya kupendeza, ni sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto.


Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!


Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada.


Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo