Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 28:15 - Swahili Revised Union Version

15 Tena mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Tena mtamtolea Mwenyezi-Mungu sadaka ya kuondoa dhambi, beberu mmoja, licha ya ile sadaka ya kuteketezwa ya kila siku na sadaka yake ya kinywaji.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Mwenyezi Mungu kuwa sadaka ya dhambi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa bwana kama sadaka ya dhambi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Tena mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA itasongezwa zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya siku zote, pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

Tazama sura Nakili




Hesabu 28:15
14 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu.


Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya kama alivyofanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema,


naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao.


akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ataleta mbuzi dume asiye na dosari awe matoleo yake;


ndipo itakapokuwa, kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu, ndipo mkutano wote utasongeza ng'ombe dume mdogo mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza kwa BWANA, pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji, kama amri ilivyo, na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi.


Tena sadaka zake za vinywaji zitakuwa nusu ya hini ya divai kwa ng'ombe, na sehemu ya tatu ya hini kwa kondoo dume, na robo ya hini kwa mwana-kondoo; hii ndiyo sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi katika miezi yote ya mwaka.


tena mtasongeza mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.


Nawe utawaambia, Hii ndiyo sadaka isongezwayo kwa moto mtakayomsogezea BWANA; wana-kondoo dume wawili wa mwaka mmoja wakamilifu, kila siku, wawe sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote.


na mbuzi dume mmoja, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.


na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji.


na mbuzi dume mmoja kuwa sadaka ya dhambi, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu;


Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;


Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo