Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 20:10 - Swahili Revised Union Version

10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kisha Mose na Aroni wakaikusanya jumuiya yote ya watu mbele ya mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni sasa, enyi waasi: Je, tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kisha Mose na Aroni wakaikusanya jumuiya yote ya watu mbele ya mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni sasa, enyi waasi: Je, tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kisha Mose na Aroni wakaikusanya jumuiya yote ya watu mbele ya mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni sasa, enyi waasi: je, tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Musa na Haruni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Musa akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Musa na Haruni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Musa akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu?

Tazama sura Nakili

Hesabu 20:10
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamwambia, Tumeota ndoto wala hapana awezaye kuifasiri. Yusufu akawaambia, Nawaomba mniambie, kufasiri si ni kazi ya Mungu?

Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani.

Akafanya vijito vitokeze katika mwamba, Na kufanya maji yatiririke kama mito.

Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.

Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.

Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.

Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.

Muwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;

Mmekuwa na uasi juu ya BWANA tokea siku nilipowajua ninyi.

Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo