Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 18:26 - Swahili Revised Union Version

26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 “Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 “Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 “Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 “Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ninayowapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kuwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu, iwe zaka ya hiyo zaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 “Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ambayo ninawapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kama sadaka kwa bwana, iwe zaka ya hiyo zaka.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.

Tazama sura Nakili

Hesabu 18:26
7 Marejeleo ya Msalaba  

Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.

Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.

Malimbuko ya unga wenu mtampa BWANA sadaka ya kuinuliwa, katika vizazi vyenu.

Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.

Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

Na sadaka yenu ya kuinuliwa itahesabiwa kwenu, kama ndiyo nafaka ya sakafu ya kupuria, na kama kujaa kwake kinu cha kusindikia zabibu.

Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika uzao wa Abrahamu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo