Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 18:1 - Swahili Revised Union Version

1 BWANA akamwambia Haruni, Wewe na wanao na nyumba ya baba zako pamoja nawe mtachukua uovu wa patakatifu; wewe na wanao pamoja nawe mtauchukua ukuhani wenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Aroni, “Lawama zote kuhusu huduma ya hema takatifu, zitakuwa juu yako, wanao na ukoo wako; kadhalika makosa yanayoambatana na ukuhani wako wewe mwenyewe na wanao mtahusika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Aroni, “Lawama zote kuhusu huduma ya hema takatifu, zitakuwa juu yako, wanao na ukoo wako; kadhalika makosa yanayoambatana na ukuhani wako wewe mwenyewe na wanao mtahusika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Aroni, “Lawama zote kuhusu huduma ya hema takatifu, zitakuwa juu yako, wanao na ukoo wako; kadhalika makosa yanayoambatana na ukuhani wako wewe mwenyewe na wanao mtahusika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mwenyezi Mungu akamwambia Haruni, “Wewe, wanao na jamaa ya baba yako mtawajibika kwa makosa dhidi ya mahali patakatifu, na wewe na wanao peke yenu ndio mtakaowajibika kwa makosa dhidi ya ukuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 bwana akamwambia Haruni, “Wewe, wanao na jamaa ya baba yako mtawajibika kwa makosa dhidi ya mahali patakatifu, na wewe na wanao peke yenu ndio mtakaowajibika kwa makosa dhidi ya ukuhani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 BWANA akamwambia Haruni, Wewe na wanao na nyumba ya baba zako pamoja nawe mtachukua uovu wa patakatifu; wewe na wanao pamoja nawe mtauchukua ukuhani wenu.

Tazama sura Nakili




Hesabu 18:1
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili vipate kukubaliwa mbele za BWANA.


Ataona mazao ya taabu ya nafsi yake, na kuridhika. Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki Atawafanya wengi kuwa wenye haki; Naye atayachukua maovu yao.


Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na BWANA ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.


Tena lala chini kwa ubavu wako wa kushoto, ukaweke huo uovu wa nyumba ya Israeli juu yake; kwa kadiri ya hesabu ya siku utakazolala juu yake, kwa kadiri hiyo utauchukua uovu wao.


Kwa nini hamkula hiyo sadaka ya dhambi katika mahali patakatifu, kwa kuwa ni takatifu sana, naye amewapa ninyi ili kuuchukua uovu wa mkutano, na kuwafanyia upatanisho mbele za BWANA?


hata wakawatwika ule uovu uletao hatia, hapo walapo vitu vyao vitakatifu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.


Basi kwa hiyo watayashika maagizo yangu, wasije wakachukua dhambi kwa hayo, nao wakafa humo, wakiyanajisi; mimi ndimi BWANA niwatakasaye.


Kwa jumla ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arubaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arubaini, nanyi mtakujua kuchukizwa kwangu.


tena ya kuwa amekuleta uwe karibu, na ndugu zako wote wana wa Lawi pamoja nawe? Nanyi, je! Mwataka na ukuhani pia?


Kila mtu akaribiaye, aikaribiaye maskani ya BWANA, hufa; je! Tutakufa sote pia?


Na katika fimbo ya Lawi utaliandika jina la Haruni; maana, itakuwa fimbo moja kwa kila kichwa cha nyumba za baba zao.


Kisha Musa akaziweka hizo fimbo mbele za BWANA katika hema ya kukutania.


Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.


Lilete karibu kabila la Lawi, ukawaweke mbele ya Haruni kuhani, ili wapate kumtumikia.


Na wakati huo BWANA alilitenga kabila la Lawi ili walichukue lile sanduku la Agano la BWANA, wasimame mbele ya BWANA kwa kumtumikia, na kuwabarikia watu kwa jina lake, hata hivi leo.


Watiini viongozi wenu, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa huzuni; maana haitawafaa ninyi.


Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa kama sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.


Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.


Basi Mika akamweka wakfu huyo Mlawi, huyo kijana, naye akawa kuhani wake, akakaa nyumbani mwa Mika.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo