Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 16:42 - Swahili Revised Union Version

42 Basi ilikuwa, hapo huo mkutano ulipokuwa umekutanika kinyume cha Musa, na kinyume cha Haruni, wakaangalia upande wa hema ya kukutania; na tazama, hilo wingu likaifunika hema, na utukufu wa BWANA ukaonekana.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Walipokusanyika mbele ya Mose na Aroni ili kutoa malalamiko yao, waligeuka kuelekea hema la mkutano, wakaona kuwa wingu limeifunika hema na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulikuwa umetokea hapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Walipokusanyika mbele ya Mose na Aroni ili kutoa malalamiko yao, waligeuka kuelekea hema la mkutano, wakaona kuwa wingu limeifunika hema na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulikuwa umetokea hapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Walipokusanyika mbele ya Mose na Aroni ili kutoa malalamiko yao, waligeuka kuelekea hema la mkutano, wakaona kuwa wingu limeifunika hema na utukufu wa Mwenyezi-Mungu ulikuwa umetokea hapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Lakini kusanyiko walipokusanyika kupingana na Musa na Haruni, nao wakageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu wa Mwenyezi Mungu ukatokea.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Lakini wakati kusanyiko lilipokusanyika kupingana na Musa na Haruni, nalo likageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu wa bwana ukatokea.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

42 Basi ilikuwa, hapo huo mkutano ulipokuwa umekutanika kinyume cha Musa, na kinyume cha Haruni, wakaangalia upande wa hema ya kukutania; na tazama, hilo wingu likaifunika hema, na utukufu wa BWANA ukaonekana.

Tazama sura Nakili

Hesabu 16:42
10 Marejeleo ya Msalaba  

Ilikuwa Haruni aliponena na huo mkutano wote wa wana wa Israeli, wakaangalia upande wa bara, na tazama, utukufu wa BWANA ukaonekana katika hilo wingu.

na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa BWANA; kwa kuwa yeye husikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia?

Na huo utukufu wa BWANA ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.

Kisha Musa na Haruni wakaingia ndani ya hema ya kukutania, kisha wakatoka nje, na kuwabariki watu; na huo utukufu wa BWANA ukawatokea watu wote.

Lakini mkutano wote wakaamuru wapigwe kwa mawe. Ndipo utukufu wa BWANA ukaonekana katika hema ya kukutania, mbele ya wana wa Israeli wote.

Kisha Kora akakutanisha mkutano wote kinyume chao mlangoni pa hema ya kukutania; na utukufu wa BWANA ukatokea mbele ya mkutano wote.

Na Musa na Haruni wakaenda hapo mbele ya hema ya kukutania.

Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakakusanyika Juu ya Musa na juu ya Haruni.

Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hadi mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo