Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Esta 6:4 - Swahili Revised Union Version

4 Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwandalia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mfalme akauliza, “Kuna ofisa yeyote uani?” Ikawa wakati huo Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa ikulu; alikuwa amekuja kwa mfalme kuomba Mordekai auawe kwenye mti wa kuulia ambao alikuwa amekwisha mtayarishia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mfalme akauliza, “Kuna ofisa yeyote uani?” Ikawa wakati huo Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa ikulu; alikuwa amekuja kwa mfalme kuomba Mordekai auawe kwenye mti wa kuulia ambao alikuwa amekwisha mtayarishia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mfalme akauliza, “Kuna ofisa yeyote uani?” Ikawa wakati huo Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa ikulu; alikuwa amekuja kwa mfalme kuomba Mordekai auawe kwenye mti wa kuulia ambao alikuwa amekwisha mtayarishia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati huo huo Hamani alikuwa ameingia kwenye ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati huo huo Hamani alikuwa ameingia ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

4 Mfalme akauliza tena: Uani yuko nani? Naye Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aje kumwambia mfalme, wamtundike Mordekai katika ule mti, aliomsimikia.

Tazama sura Nakili




Esta 6:4
12 Marejeleo ya Msalaba  

Watumishi wote wa mfalme wanajua sana, hata na watu wa majimbo ya mfalme, ya kwamba mtu yeyote, akiwa mwanamume au mwanamke, atakayemjia mfalme katika ua wa ndani, wala hakuitwa, kuna sheria moja kwake, ni kwamba auawe; isipokuwa yeye ambaye mfalme atamnyoshea fimbo ya dhahabu, ili aishi; wala mimi sikuitwa niingie kwa mfalme yapata siku thelathini.


Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa kasri.


Basi Zereshi mkewe na marafiki wote wa Hamani wakamwambia, Na kitengenezwe kiunzi cha mti wa kunyongea wa urefu wa mikono hamsini, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa furaha pamoja na mfalme karamuni. Basi ushauri huu ukamridhisha Hamani, akautengeneza mti wa kunyongea.


Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au hadhi gani Mordekai aliyofanyiwa kwa ajili ya hayo? Watumishi wa mfalme waliomhudumia wakamwambia, Hakuna alilofanyiwa.


Basi watumishi wa mfalme wakamwambia, Tazama, Hamani yupo, amesimama behewani. Mfalme akasema, Na aingie.


Ndipo aliposema Harbona, towashi mmojawapo wa wale waliohudumu mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.


Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao wenyewe; Na mashauri ya washupavu yaharibika kwa haraka.


Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.


Ili kuwaponya nafsi zao kutoka kwa mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa.


Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo