Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 9:4 - Swahili Revised Union Version

4 Nikamwomba BWANA, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuungama, nikisema: “Ee Bwana, wewe ni Mungu mkuu na wa kuogofya. Wewe ni mwaminifu kwa agano lako na unawafadhili wakupendao na kuzitii amri zako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuungama, nikisema: “Ee Bwana, wewe ni Mungu mkuu na wa kuogofya. Wewe ni mwaminifu kwa agano lako na unawafadhili wakupendao na kuzitii amri zako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Nilimwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, na kuungama, nikisema: “Ee Bwana, wewe ni Mungu mkuu na wa kuogofya. Wewe ni mwaminifu kwa agano lako na unawafadhili wakupendao na kuzitii amri zako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Nikamwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, na kutubu: “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Nikamwomba bwana Mwenyezi Mungu wangu na kutubu: “Ee Bwana, Mungu mkuu na unayetisha, anayeshika agano lake la upendo kwao wanaompenda na kutii maagizo yake,

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

4 Nikamwomba Bwana Mungu wangu nikiungana na kusema hivyo: E Bwana, ndiwe Mungu mkuu aogopeshaye, unalishika agano la kuwahurumia wakupendao na kuyashika maagizo yako.

Tazama sura Nakili




Danieli 9:4
30 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema Ee BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote.


ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.


Basi hapo Ezra alipokuwa akiomba na kuungama, akilia, na kujiangusha kifudifudi mbele ya nyumba ya Mungu, kusanyiko kubwa sana la wanaume, wanawake na watoto, kutoka katika Israeli likamkusanyikia; maana watu hao walikuwa wakilia sana.


nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake;


Basi sasa, Ee Mungu, mkuu, mwenye uweza, Mungu wa kuogofya, mwenye kushika maagano na rehema, mashaka yote yaliyotupata sisi, wafalme wetu, na wakuu wetu, na makuhani wetu, na manabii wetu, na baba zetu, na watu wako wote, tangu zamani za wafalme wa Ashuru hata leo, na yasihesabiwe kuwa ni madogo.


Ndipo nikakuungamia dhambi yangu, Wala sikuuficha upotovu wangu. Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA, Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.


nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.


Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA.


nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lolote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote;


Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.


Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kusihi kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu.


Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;


Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.


nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.


Na itakuwa, kwa sababu mnazisikiliza hukumu hizi, na kuzishika na kuzitenda, basi BWANA, Mungu wako, atakutimilizia agano na rehema aliyowaapia baba zako;


Usiingiwe na hofu kwa sababu yao; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yuko pamoja nawe, Mungu mkuu, mwenye utisho.


Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hadi vizazi elfu;


Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji la uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo